KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa:Nimesikitishwa Sana na mahudhurio ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeeo( Chadema), Dk Willbrod Slaa jana alizungumzia kukatishwa kwake tamaa na mahudhurio ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Dk Slaa alisema hayo jana wakati wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya mahudhurio kuwa hafifu.
 
Alisema asilimia 50 ya mahudhurio ya wajumbe katika jimbo hilo ni aibu na yanatia shaka iwapo wana nia ya dhati ya kushika dola mwaka 2015.
“Dalili hii inaonyesha kwamba kuna tatizo, hivyo kupitia mkutano huu tutayamaliza na kurudisha ufanisi wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii itaendelea ya wajumbe kutafutana kwa njia ya simu itakuwa hatari wakati wa kuunda baraza la mawaziri” alisema na kuongeza:
 
“Haiwezekani Rais akawa anatafuta baraza la mawaziri kwa njia ya simu, kwani bila kujipanga wakati huu itakuwa ngumu huko mbele tunakokwenda,” alisema.
Katika mazungumzo yake Dk Slaa alisema, wanakusudia kutoa tamko la nini ifanyike kuhusu mauaji mbalimbali ya wananchi yalifanywa na polisi baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwachukulia hatua Waziri wa Mambo ya Ndani , Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema na Kamanda wa Mkoa wa Iringa Michael Kamhanda.
“Hatuwezi kutulia huku tukiona vyombo ambavyo vinatakiwa kulinda usalama wa raia ndio vinakuwa vya kwanza kuwaua raia wasiokuwa na hatia huku kiongozi wa nchini (Rais Kikwete) akiwa kimya bila kutoa tamko lolote,” alisema.
 
Katika mkutano huo, wajumbe walitakiwa kufika mapema kwa ajili ya kuanza kwa mkutano saa 4 hadi saa 6 mchana, lakini kutokana na ufinyu wa mahudhurio, mkutano huo ulianza saa 6.47 mchana.
Sifa zimwendee Mwenyekiti wa Chama hicho Jimbo la Kinondoni, Deo Mushi ambaye alifanya kazi ya kuwatafuta wajumbe hao kwa njia ya simu ili kutimiza idadi ya asilimia 50.
Mratibu wa Mkutano huo, Mkurungenzi wa Sera na Utafiti wa Chama hicho, Chacha Mwita, alisema wajumbe waliokuwa wamefika walikuwa hawana uwezo wa kuruhusu kufanyika kwa mkutano huo.
Mwita alisema idadi ambayo inatakiwa ya wajumbe wote ni zaidi ya 120, lakini waliokuwa wamefika walikuwa hawazidi 50

NGASA AFUNGA GOLI 5 KILI STARS IKISHINDA 7-0 DHIDI YA SOMALIA



Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopambana na timu ay Somalia katika mchezo wa michuano ya Tusker Cecafa Challenge Cup uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda leo na kushinda kwa goli 7-0. Magoli ya Kilimanjarto Star yakipachikwa na Mrisho Ngasa (5) na John Boko (2).
Mrisho Ngassa akishangilia moja ya goli kati ya matano aliyofunga wakati wa mchezo na Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda.
Kwa hisani ya Blog ya Father Kidevu

IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA KIKAO CHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI, KENYA.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkabidhi nyundo Rais Yoweri Muzeveni kama ishara ya kukabidhi Uienyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kijana Joel Adagson Mwigomole kwa kuibuka mshindi wa pili wa kuandika Insha kwa wanafunzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa nne wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya. Joel ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mzumbe, Morogoro.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Museveni wa Uganda akimpongeza kijana Joel Adagson Mwigomole kwa kuibuka mshindi wa pili wa kuandika Insha kwa wanafunzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa nne wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya.Joel ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mzumbe, Morogoro.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia utiwaji saini mkataba wa haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya.Zoezi hili lilifanywa baina ya Mawaziri wa Bishara wa nchi wanachama wa Jumuiya na Kaimu Waziri wa Bishara wa Marekani Bi Rebecca Blank aliyehudhuria kikao hicho.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa nne wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wenzie wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na washiriki mwishoni mwa kikao cha nne cha Jumuiya nje ya Jengo la Mikutano wa Kimataifa la Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa kwa heshima wakati anaondoka jijini Nairobi, Kenya.Picha na IKULU

TASWIRA:MALI ZA MAREHEMU SHARO MILIONEA ZAANZA KUREJESHWA



Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo milionea vilivyokamatwa baada ya msako mkali baina ya Polisi na wananchi wa Kijiji Songa Kibaoni.
---
Na Mashaka Mhando,Tanga
WATU wanaosadikiwa kuiba vitu vya marehemu Hussein Mkiety maarufu kwa jina la 'Sharo Milionea' aliyefariki kwa ajali ya gari katika kijiji cha Songa Kibaoni wilayani Muheza Novemba 26 mwaka huu, wamesalimisha baadhi ya vitu hivyo kwa mwenyekiti wa Kijiji hicho huku wakiendelea kuishi mafichoni kuogopa kutiwa mbaroni.
Watu hao wamesalimisha vitu hivyo baada ya Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuwatangazia kwamba wale wote waliomwibia marehemu watasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kufutia kitendo walichokifanya kutokuwa cha kiungwana.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro,baada ya sherehe za uzinduzi wa jengo la O(fisi kuu za Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha Novemba 28, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes Amtembelea Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes mara alipomtembelea Profesa Muhongo ofisini kwake. Balozi huyo aliongozana na watendaji kutoka kampuni ya Koch Engineering & Construction ya nchini Ujerumani ambao wanania ya kuwekeza katika miradi ya nishati ikiwamo gesi asilia, umeme wa upepo, jua pamoja na kuwekeza katika viwanda vya uzalishaji mbolea.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes ramani ya bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Profesa Muhongo alimueleza mheshimiwa Balozikuwa Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi katika eneo la Somangafungu. Picha na Afisa Habari -Wizara ya Nishati na Madini.

MMILIKI WA GARI ALIYOPATA NAYO AJALI MAREHEMU SHARO MILLIONEA AJITOKEZA NA KUSEMA HAIDAI CHOCHOTE FAMILIA YA MAREHEMU


Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.

Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni jana usiku.
Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari usiku wa jana.Picha Zote na Ahmed Khatib-Tanga

MMILIKI wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.
Akizungumza kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; “Kilichotokea ni kazi ya Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu.

Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari. “Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.
Kuhusu gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.
“Kabla ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao,” alisema Suma. Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu: “Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”

TAHADHARI: UTAPELI MKUBWA WAIBUKA JIJINI DAR.

New Tannesco LUKU Sceme In Dar !

Reported by some one in the Diplomatic community.

Dear Colleagues,

Yesterday around midday, 9 men invaded my compound in Mbezi Beach while I was at work. They claimed to have come from Tanesco HQ and were there to inspect the LUKU meter. The house was locked so they could not access the meter. They harassed my guard and threatened to take him to the police station if he did not call me. The guard called me and I spoke to the men on their phone.

The purported inspector told me that they had used a GPS machine to measure the activity of my LUKU machine, and found it defective. He told me that he would assist me to correct the problem instead of referring the matter to Tanesco Office, but he needed some money to do this. I told him my guard does not keep money and asked him to come to UNICEF. He and four other men came to UNICEF but refused to enter the compound. I and one of the KK guards went out to talk to them. They asked for Tzs 3 million. I tried to get them to move closer to the gate so that people would see their faces but failed. They were very guarded and the vehicle they used had very dark tints on windows. They left after a few minutes.

I refused to give them money and they left, threatening to go and disconnect power at my house.

I called Tanesco for advice and was forwarded to the security section. The security personnel advised me not to take any action before they got here. When they arrived, I narrated the whole story to them. They were quick to point out that the inspectors were fake. Tanesco does not use GPS to measure anything. The 9 men were con-men popularly called "vishoka" who have been terrorizing Mbezi, Ubungo and Kigamboni for money. He informed me that 6 such men were caught the day before and were being held at the Central Police Station. It was his guess that the men who came to my house and that of another lady in Ubungo were looking for money to bail out their colleagues, which would explain their aggressive behavior. I gave them the phone number of the person who called...and the number plate of the vehicle.

Be careful of anyone calling himself Sadiki Kanya: 0716652020

The security personnel asked me to warn my colleagues and friends and to share the below telephone numbers. If you experience any disturbance from vishokas, please call:

Francis Maze: 0777/0762450226
Eng Sangiwa: 0765110070
Godfrey Lyimo: 0767553324
Tom: 0754984287

Please warn guards and helpers at your residence. The group barging into the compound will comprise not less than 6 people. They must be prepared not to open the gate and must call for help immediately. If the men make it into the compound, it will be virtually impossible to control the situation. They have strength in numbers. They are loud, aggressive and very well-dressed (and well-fed!), with authentic-looking Tanesco ID cards, forms, cameras etc. The was even one man bearing what looked like BBC ID, representing the media.

Taasisi ya Catherine Magige Foundation yazinduliwa jijini Arusha leo

 

Mbunge wa viti maalum vijana CCM mkoani Arusha Catherine Magige akiwa na baadhi ya vijana wakibadilishana mawazo kabla ya uzinduzi ulioenda sambamba na hafla ya utoaji wa msaada wa baiskeli za walemavu kutoka kwa Taasisi ya Catherine Foundation kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha leo Asubuhi.Picha na( Mahmoud Ahmad Arusha)

 
Mbunge wa viti maalum Bi Catherine Maggige akisomama taarifa ya aasisi yake ilivyoanza kazi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wa Catherine Foundation kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha leo Asubuhi
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akiwa na mbunge wa viti maalum Bi. Catherine Maggige wanawakabidhi zawadi ya baiskeli kwa walemavu watatu kwa niaba ya walemavu 20 waliopewa baiskeli hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. John Mongela akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Arusha