Gari
aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa
akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo
Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga
Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na
mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Baadhi
ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za
usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki
Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam
kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo
Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule
Muheza Tanga.
Gari
aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa
akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo
Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga
Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na
mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Mbunge
wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha
Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia
mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati
akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo
imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni jana usiku.
Wakazi
wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba
cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo
Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari usiku wa jana.Picha Zote na
Ahmed Khatib-Tanga
MMILIKI
wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan
‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza,
Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza
uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.
Akizungumza
kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka
malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; “Kilichotokea ni kazi ya
Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu.
Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari. “Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.

Kuhusu
gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga
kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.
“Kabla ya
kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo.
Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima
kuzungumza nao,” alisema Suma. Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine
atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye,
alijibu: “Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”
Kabla ya ajali.
Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri. “Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,” alisema Suma na kuongeza:

“Tulianza
kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia
hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni,
akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi
jaribu kuwa mwangalifu sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua.
Tukakubaliana kwamba atakaporudi aende hospitali kucheki afya
yake.”
Kuhusu
uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: “Mimi ni mfanyabiashara na yeye alikuwa
msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka ikafikia wakati nikaona kuwa
ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua kama sehemu ya familia.”
Alisema
marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya kwenda nalo
Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu.“Siyo mara ya kwanza kuitumia gari
lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya kwanza alichukua na kusafiri nalo
mwenyewe, halafu safari ya pili ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu,” alisema
Suma.
Eneo la
ajali wakimbia makazi Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako
Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya
ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo
kuzisalimisha mara moja.
No comments:
Post a Comment