DK. HARRISON MWAKYEMBE APOKEA TAARIFA YA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA UTENDAJI KAZI WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA).

 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Bw Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya kuchunguza utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).Waziri wa Uchukuzi ameiahidi Kamati kuwa kila kipengele walichoshauri kwenye ripoti hiyo kitachukuliwa hatua na Mpaka Disemba mwaka huu Utekelezaji wa Mapendekezo ya ripoti yatakuwa yametekelezwa yote.
 Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Bernard Mbakileki akionyesha Magazeti mbalimbali kwa Waziri wa Uchukuzi,Watendaji wa taasisi za Wizara Uchukuzi pamoja na waandishi wa habari hawapo pichani yaliyokuwa yakiripoti mambo mbalimbali wakati uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.

 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Benard Mbakileki,Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari(hawapo Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu wanane aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa mapendekezo yalioandikwa kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila aliyehusika na ubadhilifu atachukuliwa hatua.

VERY IMPORTANT;TAHADHARI KUHUSU MABOMU 30 TOKA MALAWI

Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu.
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.


Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.


Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.

SHYROSE BHANJI ALETA TAFRANI KWENYE UCHAGUZI WA UWT, NUSUSA APATE KIPIGO KUTOKA KWA WAPAMBE WA SOPHIA SIMBA.


 Shyrose akikwaruzana na wapambe wa Sophia Simba ambaye ni Mgombea wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania.
 
Jana wakati wa uchaguzi wa jumuiya ya wanawake wa CCM nusura uchaguzi huo uingie doa baada ya tafrani kutokea pale Mh. Mbunge wa Jumuiya ya Afrika mashariki Shyrose Bhanji alipomuuliza swali mgombea wa kiti cha Uenyekiti wa jumuiya hiyo Mh.Sophia Simba kutaka kujua kama kiongozi huyo wakati wa utawala wake wa jumuiya hiyo alijitahidi kiasi gani kuifanya jumuiya hiyo iweze kuongeza wanachama!! na kujikuta Mh. Shyrose akiambulia jibu la kuambiwa yeye ni mgeni kwenye jumuiya hiyo na hajui lolote.
Jibu hilo inaonekana halikumridhisha Mh. huyo wa Afrika mashariki na kuamua kumfuata Mgombea baada ya kushuka na kurushiana naye maneno ya kashfa mpaka palewatu wa usalama walipotokea na kuituliza tafrani hiyo kwa kumtoa nje Mh. Shyrose na mambo mengine kuendelea.
Hata hivyo Mh. Simba alishinda Uchaguzi huo kwa mara nyingine katika ngazi ya Uenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa.

YANGA WAKABIDHIWA JEZI ZA DOA JEUSI WALIZOTAKA

 Meneja Mahusiano ya Nje wa kampuni ya Sima za mkononi VODACOM, Salum Mwalimu akionesha jezi walizokabidhi kwa klabu ya Yanga zikiwa na doa jeusi. (Picha na Habri Mseto Blog)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Laurence Mwalusako (kati) akipokea jezi walizokabidhiwa na Vodacom zikiwa na doa jeusi kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa kampuni ya Sima za mkononi VODACOM, Salum Mwalimu (kushoto). Kulia ni Ofisa Udhamini wa kampuni hiyo, Ibrahim Kaude
Ushauri wa kizushi: Kuna Mdau anashauri wana Yanga hata kama Vodacom wakiwapa hela za kuendeshea timu katika msimu wawape masharti ya kuto kuwapa NOTI ZA ELFU KUMI kwa sababu ni nyekundu na masharti hayo pia wakilipwa kwa cheki wakienda Benki wakatae noti hizo wachukue noti za  jelo jelo tu .
Fukuto kubwa limeanza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, kutokana na baadhi ya wanachama kuhoji uhalali wa ukoo wa Kikwete kushika nafasi nyeti karibu zote katika Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo.

Ukoo huo umehakikisha unashika nafasi zote za juu, ikiwamo ya Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo iliyokwenda kwa Shaibu Mtawa.
Mtawa alipata kura 811 na kumshinda Mohamed Mrisho Kikwete aliyepata kura 613. Mtawa na Mohamed wote ni ndugu wa damu wa Rais Kikwete.
Habari za uhakika kutoka miongoni mwa wanachama, zinasema majina ya wanandugu hao yalipendekezwa kutoka miongoni mwa wanachama 13. Wengi wao walikatwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na kuhitimishwa kwenye vikao vya kitaifa ambavyo Mwenyekiti wake ni Rais Kikwete.
Katika ngazi hiyo ya Taifa, Mwenyekiti Kikwete alihakikisha majina matatu yanarejeshwa. Mawili - Shaibu na Mohamed - yakiwa ni ya ndugu zake, na mwingine Omar Mhando.
“Mhando hapa aliwekwa kama msindikizaji kwa sababu kwenye raundi ya kwanza aliangushwa. Kwa kuwa hakuna mgombea aliyepata nusu ya kura, ikabidi upigaji kura urudiwe. Ikawa hivyo kwa kupigia majina mawili ya ndugu.
“Kilichofanyika kwenye uenyekiti ni kuhakikisha majina mawili ya wanandugu hawa yanaingia ili mmoja achaguliwe. Hilo limewezekana kwa kuchaguliwa Shaibu,” amesema mmoja wa wanachama.
Habari za uhakika zinasema kwamba kwenye uchaguzi huo kulikuwa na mvutano mkali kati ya wanandugu, hasa kutokana na ukweli kwamba Shaibu ni mdogo wa Katibu Msaidizi wa Rais Kikwete, Alhaji Kassim Mtawa.
“Mvutano ulikuwa mkali kweli kweli bila kujali kuwa waliokuwa wakigombea ni wanandugu, ulikuwa mchuano wa miamba,” kimesema chanzo chetu cha habari.
Baada ya uchaguzi huo, siku iliyofuata wanandugu walikutana katika kikao cha ukoo, kwa ajili ya kuzika tofauti zilizojitokeza miongoni mwao wakati wa uchaguzi.
Mohamed Kikwete anakaririwa kusema kwamba hakuwa na kinyongo kutokana na kushindwa na Mtawa.
“Aliyeshinda ni mdogo wangu, sina kinyongo,” alikaririwa akisema.
Baadaye kilifanyika kikao cha Halmashauri Kuu kwa ajili ya kumchagua Katibu Uenezi na Katibu wa Uchumi.
“Kabla ya uchaguzi, wapigakura kadhaa waliwekwa sawa, kuna kina mama walipata khanga, kina baba wakapata misuli na fedha za usafiri. Wajumbe walikuwa kama 140. Sikusikia aliyenung’unika kuwa amekosa kitu,” kimesema chanzo chetu.
Katika nafasi ya Katibu Uenezi, mshindi alikuwa ni ndugu mwingine kutoka ukoo huo huo wa Kikwete, aliyetajwa kwa jina la John Francis (Boli Zozo).
Kana kwamba hiyo haikutosha, nafasi ya Katibu Uchumi Wilaya ya Bagamoyo akachaguliwa Iddi Swala. Huyu ni mjukuu wa Rais Kikwete kwani amezaliwa na mtoto wa dadake Rais.
Ushindi wa Swala umezua gumzo kubwa hasa kutokana na namna alivyokuwa kiongozi ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo. Mgombea aliyetajwa kwa jina moja la Mtiga, aliyeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa uongozi, alishindwa.
Awali, ndugu mwingine wa Rais Kikwete aitwaye Yusuf Mrisho Kikwete, alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Kata ya Dunda, Bagamoyo.
Kuchaguliwa kwa wanaukoo hao, pamoja na kupita bila kupingwa kwa Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete, kunaifanya Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Bagamoyo iwe na viongozi wakuu wanne ambao ni ndugu wa damu, pamoja na wajumbe wengine wa kawaida. Nafasi hizo ni Mwenyekiti, Mjumbe wa NEC Taifa, Katibu wa Uchumi na Katibu Uenezi.
Hata hivyo, kuwapo kwa wanandugu hao kungeweza kupanuka zaidi endapo nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Bagamoyo, ingeshikwa na mwanaukoo mwingine wa Kikwete, Magreth Halfan Kikwete. Magreth kaolewa na mtoto wa Mzee Seleman Kikwete.
“Huyu wanachama wakasema haiwezekani, wakaamua kumbwaga maana ilishaonekana sasa chama kinakuwa cha ukoo tu. Tukaamua kumpa Hapsa Kilingo,” amesema mwanachama mwingine.
Kadhalika, ndugu mwingine wa Rais Kikwete, Mwanaisha Halfani Kikwete, alipitishwa kugombea Ujumbe Baraza Kuu/Halmashauri Kuu ya UWT Mkoa wa Pwani.
Wakati hali ikiwa hivyo kwenye uchaguzi huu unaoelekea ukingoni, mtoto mwingine wa Rais Kikwete, Khalfan Kikwete ni Mjumbe wa Baraza Kuu Idara ya Chipukizi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Mwenyekiti wa Idara hiyo ni Gabriel Makalla - mtoto wa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
 
Ushindi wa Ridhiwani, Mama Salma
Kitendo cha Ridhiwani kupita bila kupingwa kumeacha maswali mengi. Kuna habari kutoka kwa baadhi ya wanachama kwamba wale waliothubutu kujitokeza kuwania nafasi hiyo walitishwa, na wao wakatishika.
Wapo wanaosema kwamba kupita kwake kwa mbinu hiyo kulitokana na hofu ya wajumbe kutokana na ukaribu alionao na mzazi wake, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Ni woga kama huo uliowaingia pia wanachama na wapenzi wa CCM katika Wilaya ya Lindi Mjini, walioamua kusalimu amri na kushuhudia mke wa Rais Kikwete, Mama Salma, akipita bila kupingwa.
Ridhiwani na ubunge 2015
Watu walio karibu na kijana huyo wanasema kwamba anajiandaa kugombea ubunge Jimbo la Bagamoyo mwaka 2015.
Wanaotoa madai hayo wanatetea hoja yao kwa kigezo cha namna Kamati ya Wilaya ilivyosukwa kwa kuwa na viongozi wakuu ambao karibu wote ni ukoo mmoja. Wachunguzi wa mambo wanasema matumaini ya Mbunge wa sasa wa Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa, kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 yamefutwa kutokana na kundi lake kushindwa vibaya katika ngazi karibu zote.
Kwa sasa Dk. Kawambwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Jambo jingine ambalo JAMHURI haijalithibitisha ni kwamba suala la ukabila nalo limekuwa likitawala kwenye uchaguzi wilayani Bagamoyo, kama ilivyo kwenye uchaguzi wa CCM katika maeneo mbalimbali nchini.
Dhambi hiyo ndiyo inayomfanya Dk. Kawambwa sasa aonekane kuwa ‘wa kuja” asiyetakiwa na “wazawa”.
Mbona hata Nyerere alipendelea?
Kuna hoja zinazojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, naye alipendelea ndugu zake wakati akiwa katika uongozi.
Anatajwa Joseph Warioba Butiku, aliyekuwa Katibu Myeka wa kiongozi huyo, kama kielelezo cha Mwalimu kuwabeba ndugu.
Pia anatajwa Joseph Nyerere, ambaye ni tumbo moja na Mwalimu, aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa muda usiozidi miaka miwili; na pia Katibu wa Umoja wa Vijana wa TANU.
Baadaye, kuanzia miaka ya 1970 hadi kifo chake miaka ya 1990, Joseph alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Butiama.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali David Musuguri, naye anatajwa kama mmoja wa waliopendelewa na Mwalimu, ingawa kumbukumbu zinaonesha kuwa Janerali huyo alijiunga katika Jeshi la Kikoloni la KAR kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-1945).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
 

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.

Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) yatembelea Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere

Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mhe. Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
 Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.
 Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha.

 Katibu Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho.

Kamati ya Bunge ya ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) yatembelea Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere

Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mhe. Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
 Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.
 Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha.

 Katibu Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho.

Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Apatikana

Sheikh Farid, akipokewa na ndugu na jamaa nyumbani kwake
Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho visiwani Zanzibar, Sheikh Farid, (Wapili kushoto), akipiga picha ya ukumbusho na familia yake mara baada ya kjuwasili nyumbani kutoka kusikojulikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012



Sheikh Farid, na baadhi ya wafuasi wake, wakiomba dua nyumbani kwake mara baada ya kupatikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012-
--
Kuna habari kuwa kiongozi wa Jumuiyab ya Uamsho, kisiwani Unguja, Zanzibar, Sheikh Farid amepatikana nay u salama salimin.

Picha za mitandao zinaonhyesha sheikg huyo mwenye msimamo makali alionekana akilakiwa na watu b waliotajwa kuwa ni ndugu na jamaa, ambapo picha nyingine zinaonyesdha akiwa na familia yake na moja ikionyesha akiomba dua nyumbani kwake.
Kwa mjujibu wa taarifa za mkitandao, Sheikh huyo aliyetoweka tangu Oktoba 16, 2012 na kuonekana tena Oktoba 19, 2012 majira ya jioni, alisema, “alichukuliwa na watu waliojitambulisha kwake, kuwa ni askari polisi na baadhi yao wakiwa na silaha.”.Alisema

|Nilifungwa kitambaa cheusi usoni na kupelekwa nisikokujua” alifafanua sheikh huyo.

Amedai askari hao wenye lafudhi za Tanzania Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano yake na baadhi ya viongozi wa serikali.

Pia askari hao walichukua simu yake na kumuhoji mengi kuhusu namba na message zilizopo kwenye simu yake. Watu hao walimrudisha eneo walilomchukua wakamfungua pingu na kitambaa cha usoni kisha wakamuachia huru.

Alisema watu hao waliomchukua kwa gari walikuwa wanne, akiwepo dereva na mwingine aliyekaa mbele ambaye alijitambulisha kwake, na nyuma ya gari walikuwepo watu wawili waliovaa kofia zilizofunika nyuso zao.




Kiundani Tuzo hizi zinaitwa ‘Mo Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership’ ambzo hutolewa
na Taasisi ya ‘Mo Ibrahim Foundation’ kwa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika ambao wamefanikisha utekelezaji katika Nyanja ya Ulinzi, Afya, Elimu na Maendeleo ya Uchumi katika nchi zao na ambao wameachia madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Sasa ndugu zangu ya kwanza mwaka 2007 ilikwenda kwa aliyekuwa rais wa Msumbiji Joaquim Chissano kwa kuiongoza nchi hiyo kutoka katika mifarakano na kuwa ya Kidemokrasia.
2008: Tuzo hiyo alipewa Rais Festus Mogae wa Botswana kwa uongozi wake kuwezesha taifa hilo kusimama dhidi ya vita ya maambukizi ya Ukimwi ambayo yalikuwa yakitishia ustawi wa taifa hilo.
2009 na 2010: – Alikosekana Mshindi.
2011: Tuzo hiyo ilikwenda kwa kiongozi wa Pedro Pires wa Cape Verde.
2012: Tena amekosekana Mshindi.