Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison
Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Bw
Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa
tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya kuchunguza utendaji kazi wa Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA).Waziri wa Uchukuzi ameiahidi Kamati kuwa kila
kipengele walichoshauri kwenye ripoti hiyo kitachukuliwa hatua na Mpaka
Disemba mwaka huu Utekelezaji wa Mapendekezo ya ripoti yatakuwa
yametekelezwa yote.
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa
kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw.
Bernard Mbakileki akionyesha Magazeti mbalimbali kwa Waziri wa
Uchukuzi,Watendaji wa taasisi za Wizara Uchukuzi pamoja na waandishi wa
habari hawapo pichani yaliyokuwa yakiripoti mambo mbalimbali wakati
uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison
Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati
hiyo Bw Benard Mbakileki,Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri
huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt.
Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari(hawapo
Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu wanane aliyoiunda
kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA).Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa mapendekezo yalioandikwa
kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila aliyehusika na ubadhilifu
atachukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment